Monday 25 December 2017

Waliberia kufanya uchaguzi wa rais baada ya Krismas



Waliberia watamchagua kiongozi mpya Jumatano (27.12.2017) katika uchaguzi wa duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na mchezaji kandanda wa zamani maarufu George Weah.
Kura hiyo itaashiria mabadiliko  ya  kwanza  ya uongozi  nchini  humo  tangu  mwaka  1944.
Baada  ya  wiki  saba  za uchelewesho kutokana  na  malalamiko  ya kisheria  yaliyofikishwa  mahakamani  na  chama  tawala  cha Boakai  cha  Unity dhidi  ya  tume  ya  uchaguzi  nchini  humo, vituo vya  kupigia  kura  vinatarajiwa  kufunguliwa  kuanzia  saa  mbili asubuhi  saa  za  Liberia  na  kufungwa majira  ya  saa  12  jioni  kwa ajili  ya  wapigakura  milioni 2.1 waliandikishwa  kupiga  kura.
Liberia Monrovia Wahlen (Getty Images/AFP/I. Sanogo) Kitambulisho cha mpiga kura nchini Liberia
Chama  cha  Weah cha  Muungano  kwa  ajili  ya  mabadiliko  ya kidemokrasi, Coalition for Democratic Change (CDC) kimewataka wapiga  kura  kutokunywa  pombe kupita  kiasi  katika  sikukuu  ya Krismasi na  kuamka  mapema  siku  ya  tarehe  26  kupiga  kura zao  katika  kile  mwenyekiti  wa  tume  ya  uchaguzi  ya  taifa  NEC, Francis Korkoya  alichosema  kuwa  ni "kujitolea  mhanga  kwa  ajili ya demokrasia  yetu  na  nchi  yetu."
Watachagua  mrithi  wa  rais Ellen Johnson Sirleaf, anayetarajiwa kuondoka  madarakani  mwezi  Januari  baada  ya  miaka  12 akiwa katika uongozi  wa  juu  wa  taifa  hilo  la  Afrika  Magharibi, linaloibuka  kutoka  katika  mavumbi  ya  vita  vya  wenyewe  kwa wenyewe,(1989-2003) na pia kushughulikia hatua za kupambana  na mzozo  wa  ugonjwa  wa  Ebola (2014-16).
George Weah (Chris Hondros/Getty Images) Mchezaji soka wa zamani Goerge Opuku Weah mgombea urais Liberia
Duru  ya  kwanza
Katika  duru  ya  kwanza  ya  upigaji  kura  tarehe 10 Oktoba, Weah alipata   asilimia  38.4  ya  kura  wakati  Boakai  alikuwa  wa  pili akipata  asilimia  28.8, na  kuzusha  hatua  ya  duru  ya  pili  ya uchaguzi  kwa  kuwa  hakuna  kati  ya  wagombea  hao  wawili aliyeweza  kufikisha  idadi  ya  asilimia  50  ya  kura  inayohitajika kushinda moja  kwa  moja.
"Matokeo  yatakuwa yanakaribiana  sana,"  amesema  Ibrahim Al-Bakri Nyei, mchambuzi  wa  masuala  ya  siasa  nchini  Liberia katika  shule  ya  mitaala ya  masuala  ya  mashariki  ya  kati  na Afrika  katika  chuo  kikuu  mjini  London (SOAS), akisema  Weah alikuwa  katika  nafasi  kama  hiyo  katika  uchaguzi  wa  mwaka 2005  wakati  aliposhindwa  licha  ya wengi  kutabiri kwamba atashinda. Kutokana  na  siku  ya  uchaguzi, "inawezekana  kuwapo idadi  ndogo  ya  watu watakaopiga  kura  kuliko uchaguzi  wa kwanza,"  alitabiri.
Akisifu mchakato  usiokuwa  na  ghasia  wa  uchaguzi  hadi  sasa, Sirleaf  alisema  katika  hotuba  yake  hivi  karibuni  kwamba "uchaguzi  umechukua  nafasi  ya  risasi na mizozo  ya  uchaguzi inatatuliwa kupitia  mahakama", ikiwa  ni  ishara  ya umbali  gani Liberia  imetoka  tangu  wakati  wa  vita.
Mahakama haikuweza kuthibitisha mapungufu
Chama  cha  Unity  cha  Boakai kimejiunga  na  chama  cha  upinzani cha  Liberty kupambana  na  kile  alichosema "mapungufu  makubwa na  udanganyifu" katika  matokeo  ya  uchaguzi, lakini  mahakama kuu iligundua  kuwa  madai  hayo  hayakuweza  kuthibitishwa, na waangalizi  walitangaza  kuwa  uchaguzi  huo  ni  wa  kuaminika.

0 comments:

Post a Comment