Vijana wawili wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini
Kenya ni miongoni mwa wanafunzi waliopata maksi za juu katika mtihani wa
kitaifa wa Sekondari (KCSE) na kujizolea alama ya B+ licha ya
kukabiliwa na changamoto nyingi zilizoko kwenye kambi za wakimbizi.
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa vijana hao
Abdiweli Jama and Abdirahman Hussein waliletwa kambini miaka 11
iliyopita baada ya kutoroka vita iliyoisambarartisha nchi ya Somalia kwa
miongo kadha.
Kwa upande wake Shaffe Abdullahi, ambaye ni mwenyekiti wa shule ya waberi, ambapo vijana hao walikuwa wanafunzi, anadai kuwa “ukosefu wa walimu , vifaa vya kusomea na hali ngumu ya maisha kambini zilikuwa ni changamoto za kutosha kwa wahitimu hao…. Hata hivyo matokeo mazuri ya vijana hao yametufurahisha.
Ameongeza kuwa: “Wanafunzi wengi hufanya vizuri katika masomo yao lakini hubakia kambini kwa kukosa msaada wa kujiunga na vyuo vikuu na hulazimika kufanya kazi ya ualimu katika shule za wakimbizi japokuwa hawajapata mafunzo yoyote ya ualimu… hivyo basi tunatoa wito kuwa tunaomba msaada ili wanafunzi hawa waliofanya vizuri watimize ndoto yao.”
CHANZO VOA
0 comments:
Post a Comment