Saturday 30 December 2017

Watu 9 wafariki baada ya shambulizi Misri

 Watu tisa wamefariki baada ya shambulizi la bunduki lililotokea katika kanisa moja kusini mwa mji mkuu Cairo.

Watatu ya waliouawa ni maafisa wa polisi waliokuwa katika zamu katika kanisa la Mar Mina.
Mshambuliaji mmoja aliuawa na mshipi wake uliojaa vilipuzi kutibuliwa.
Mpiganaji mwengine alifanikiwa kutoroka.
Huduma za usalama zilitangaza mipango wiki hii ya kulinda sherehe wakati wa mwaka mpya na Krisimasi ya kanisa la Coptic.
Walipanga kupeleka kikosi cha kukabiliana na dharura.

Shambulio hilo la siku ya Ijumaa lilifanyika wakati ambapo maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria nje ya kanisa hilo walikutana na watu wawili waliowashuku, kulingana na mwandishi wa BBC mjini Cairo Radwa Gamal.
Waliwakaribia watu hao wawili ambao walianza kwa kuwafyatulia risasi polisi hao.
Kuna ripoti kwamba watu kadhaa walijeruhiwa ,wawili vibaya.

0 comments:

Post a Comment