Wednesday 6 December 2017

Wema asema ya moyoni



Msanii wa Bongo Wema Sepetu kurudi CCM kutokea Chadema, hatimaye  amevunja ukimya na kufunguka ya moyoni.

Wema amesema hawezi sana kulizungumzia hilo kwa sababu maamuzi yalishafikiwa lakini anajihisi kukatishwa tamaa.

“Yaani it so complicated najikuta sipo kwenye position ya kuielezea in simple English or Swahili, siwezi lakini tubaki tu tunaomba Mwenyenzi Mungu kwamba everything it will be ok one day inshallah” Wema ameiambia K Fm, Rwanda.

“I am strong, nisingekuwa strong nisingekuwa hapa sasa hivi najaribu kusali kwa hii hali, muda mwingine kama bidamu inakuwa inanivunja moyo najihisi nimekatishwa tamaa, yaani ok!  acha nimuachie Mungu” ameongeza.

February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi alitangaza kurudi CCM.

0 comments:

Post a Comment