Serikali
imekemea baadhi ya wawekezaji wanaotumia vibaya jina la Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwatoa wananchi katika maeneo
yao kwa kisingizio cha kupewa kibali na wizara hiyo wakati sio kweli.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi William
Lukuvi ambapo amewaonya baadhi ya wawekezaji ambao wameonekana
kushirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali katika kunyang'anya haki
za wananchi kitendo ambacho amesema kwa utawala wa serikali hii ya
awamu ya tano hakina nafasi.
Ameongeza
kwamba, kwa sasa serikali inaendelea na zoezi la kurudisha ardhi ya
wananchi mikononi mwao bila ya gharama yeyote na kwa yale maeneo ambayo
yatabainika kuwa na ukiukwaji wa umiliki watayarudisha kwa wenyewe ili
kuendelezwa.
Mh.
Lukuvi amesema zoezi la utambuzi wa umiliki wa maeneo na urasimishaji
ni endelevu kwa mikoa yote nchini lengo ni kujua maeneo yanayomilikiwa
kihalali na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imeonekana bado ni
changamoto kwa maeneo mengi mijini na vijijini.
0 comments:
Post a Comment