Friday 8 December 2017

Zambia yawataka wafanyakazi wa TAZARA kurejea kazini

Serikali ya Zambia imewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kurejea kazini wakati malalamiko yao yanafanyiwa kazi.
Jumanne wiki hii, wafanyakazi wa TAZARA upande wa Zambia walianza mgomo kushinikiza malipo ya mshahara wa miezi miwili ya Oktoba na Novemba, hivyo kusimamisha operesheni kwa upande wa Zambia huku upande wa Tanzania shughuli zikiendelea kama kawaida.
Lakini waziri wa kazi na usalama wa jamii Joyce Simukoko amesema, wafanyakazi hao wanapaswa kuendelea na kazi kwa kuwa fedha kwa ajili ya miezi hiyo miwili imeshatolewa. Amesema Wizara ya Fedha imetoa dola za kimarekani milioni 1.2 ili kulipa mishahara hiyo.

0 comments:

Post a Comment