Sunday 28 January 2018

RASHFORD NA MANENO YA GENERALI ALFRED




RAPHAEL MWENDA.
      MNAMO miaka ya 1800 Generali wa jeshi la marekani General Alfred Williams aliwahi kuwauliza wanajeshi wake 'mnaamini hapa duniani ni kitu gani kinaenda kasi sana' mmoja wao alijibu ni risasi iliyo kasi kuliko na mwingine akasema ni ndege ya kivita hahaha,alifurahi kusikia majibu yale na akauliza tena ni nani aijuaye dakika yake moja ijayo? Hakuna alieinua kinywa chake na kujibu, kisha akaendelea "kumbe maisha pekee ndiyo yaliyo kasi kuliko kitu kingine duniani".

      Miaka zaidi ya mia moja toka General Alfred atoe kauli ile kuna binadamu ajulikanae kama Marcus Rashford kila aingiapo ndani ya gari yake hulia na kutamani maisha yarudi nyuma lakini la haitawezekana.

        Mwaka 2016 baada ya majeruhi ya Anthony Martial katika mchezo wa Europa ligi Marcus aliaminiwa na aliekua kocha wa Manchester United Louis Van Gaal,aliaminiwa katika mechi ambayo hakuna shabiki alietamani kuiona sura yake,man united walihitaji ushindi kuliko kitu chochote katika mechi hii,lakini katika uajabu wa maisha Rashford aliibuka kuwa shujaa katika mchezo huu,kuazia pale aliendelea kufunga na kujizolea umaarufu kila kona ya dunia,ni nani alietamani kuona kikosi cha Manchester United kikiingia uwanjani bila jezi namba 39?nani angefurahi kuona mabeki wenye roho mbaya wa ligi kuu ya uingereza wakimchezea rafu mbaya Rashford?hata nahodha wa wakati huo Wayne Rooney asingependa hilo litokee,shabiki gani wa soka na mpenzi wa Manchester United ambae alifurahia Rashford  kumuona Rashford akitoka nje katika mchezo wa fainali wa kombe la FA baada ya kuumia,wengi walishika vichwa na hata kumsahau Anthony Martial mchezaji aliewafikisha fainali kwa goli lake la dakika za mwisho dhidi ya Everton pale pale Wembley.

Hatimae Van Gaal akafukuzwa na Jose Mourinho akakabidhiwa timu hyo,wengi wakaamini Rashford hatopata nafasi kutokana na sera za kocha huyo kuto abudu sana vijana,lakini ni nani alieisahau jioni ile pale KCOM Stadium Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic pamoja na Paul Pogba wote walishindwa kuipatia Manchester United walau goli moja,hatimae Mourinho anamnyanyua Rashford na anakwenda kuipatia timu goli la ushindi,nani alimuwaza tena Anthony Martial ni nani alijaribu kumfikiria Jesse Lingard jibu ni rahisi tu hakuna.

  Lakini kama alivyosema General Alfred mnamo mwezi march mwaka 2017 maisha ya Rashford yalibadilika pale Stanford Bridge katika usiku wa FA cup dhidi ya Chelsea, Zlatan akitumikia adhabu ya kufungiwa Anthony Martial akiuguza majeraha Wayne Rooney akiwa katika kiwango kibovu katika maisha yake ya soka timu ikiwa imeelemewa wakiwa pungufu uwanjani baada ya Ander Hererra kulimwa kadi nyekundu Manchester United walipata nafasi moja tu katika mchezo ule ulioisha kwa kufungwa goli moja bila,nafasi hii ambayo Rashford aliichezea iliwarudisha mashabiki wa Manchester nyumbani vichwa chini.

    Huo ulkua mwanzo tu he ni nani aliesahau usiku ule wa Stockholm Wayne Rooney akitupwa benchi na Rashford kuongoza mashambulizi, sina kumbukumbu nzuri ya shuti lake lililo lenga lango katika usiku ule kule Sweden. Hatimae miezi ikapita bila Rashford kubadili aina ya uchezaji ya "Mimi" na kucheza kwaajili ya timu. 

   Kasi na uharaka wa maisha aliousema Alfred unakuja hapa. Anthony Martial anafunga na kutengeneza nafasi nyingi Jesse Lingard anafunga na kuipandisha timu kwa kasi Juan Mata anaituliza timu na kuichezesha vizuri katika kundi hilo hilo anaongezwa Alexis Sanchez.hakuna binadamu angetamani kuishi katika msitu huu uliojaa wanyama wakali na wanye njaa kali mno,nani atoke ili Rashford apate nafasi ya kuonyesha uwezo wake? Shabiki gani atamsamehe Jose Mourinho kwa kumuacha Lingard nje na kumuweka ndani Rashford? 

   Namuona Rashford akitoka Carrington na tabasamu baada ya mazoezi lakini namuona akilia na kuilaani kasi hii ya maisha kila akiingia ndani ya Porsche yake anatamani nyakati zirudi nyuma atumie vizuri nafasi alizozitoa kafara atamani muda urudi nyuma atoe tena pasi nzuri ya goli anatamani kila jambo lililopita lakini wapi mshale wa saa katu hauwezi kurudi nyuma.

  Ni wakati sasa wa kutulia na kujirekebisha na kujua wapi makosa na kujifunza pia kwa wale wanaopata nafasi sasa. June mwaka huu pale Russia kutakua na sherehe na ndoto ya kila mwanasoka anaetamani mafanikio, kombe la dunia nani asitamani kuonekana na maelfu ya raia wa dunia hii? Namuona Gary Southgate akimuangalia Jesse kama mkombozi wa Uingereza huku peni yake na mkono vikiwa mashavuni akitafakari kuliandika jina la Marcus Rashford ama la. 

           Jose Mourinho analalamikiwa sana kwa falsafa zake za kutoamini vijana nae ameamua kuvua na kutua zigo la lawama na kumpa nafasi Rashford kila mechi ya Manchester United msimu huu naona akiwa ameamua kuwaonyesha mashabiki na viongozi kuwa anawaamini vijana ndio maana Anthony Martial (21) anapata nafasi Jesse Lingard (24) anapata nafasi pia lakini Rashford hataki kuitumia nafasi huyo na kuikosesha timu ushindi mara kadhaa, Mara ngapi mashabiki wa Manchester United wamemzomea Marcus? Maisha ama kweli yapo

0 comments:

Post a Comment