Mazungumzo baina ya Arsenal na
Borussia Dortmund yanaelezwa kuendelea vyema na kwamba huenda
zikakubaliana juu ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Gabon Pierre
Emerick Aubameyang.
Imefahamika kuwa Arsenal wamekuwa wakiwinda saini ya mchezaji huyo kwa muda mrefu lakini maombi yao yalikuwa yakikataliwa na Dortmund kwa kuwa hawakufikia vigezo ikiwemo dau la Pauni milioni 60, linalodaiwa kuwa huenda sasa wakatoa, ili kumnyakua kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa.
Wakati huo huo, hatma ya mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ya kuihama klabu hiyo itajulikana endapo suala la Aubameyang likikamilika.

0 comments:
Post a Comment