Wednesday 31 January 2018

Aubemeyang atinga Arsenal


Uhamisho wa mshambuliaji wa Gabon, Pierre- Emerick Aubameyang kutoka Klabu ya Borussia Dortmund kwenda Arsenal, umekamilika baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya Pauni milioni 52.7.

Klabu ya Borussia Dortmund imethibitisha uhamisho huo kupitia Mkurugenzi wake wa michezo, Michael Zorc aliyesema anamshukuru mchezaji huyo kwa mafanikio aliyoyaleta Dortmund licha ya matukio yasiyofurahisha yaliyotokea siku za karibuni

Aubameyang anafika katika klabu hiyo ya London akiwa katika kiwango cha kutisha cha kupachika magoli, akiwa amefunga magoli 100 katika mechi 119 alizochezea Dortimund kuanzia msimu wa 2016/2017

0 comments:

Post a Comment