Licha ya klabu ya Chelsea kuongoza
kwa muda mrefu zaidi kuliko wapinzani kwenye mechi ya jana ya nusu
fainali ya kwanza ya kombe la ligi nchini Uingereza, imeshindwa kuondoka
na ushindi ilipocheza dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Stamford
Bridge.
Kocha mkuu wa Chelsea, Antonio Konte, amesema sare hiyo inawapa
changamoto kuelekea mechi ya marudio watakapokuwa ugenini kwani
watalazimika kucheza kama fainali ili kusawazisha makosa ya mechi ya
jana.
Timu hzio zinatarajiwa kurudiana Januari 23, na Chelsea wanasaka kwa udi na uvumba kombe hilo ambalo hawajakuwa na bahati nalo, huku Arsenal nao wakiamini kuwa ndilo tumaini pekee lililobaki, kutokana na nafasi kuwa finyu katika ligi kuu, hukuwakiwa wameondolewa kwenye mashindano ya kombe la FA.
Mshindi wa mechi ya nusu fainali hii atakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Manchester City na Bristol City.

0 comments:
Post a Comment