Benki ya dunia imepandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka huu hadi asilimia 3.1, na kusema ukuaji mpana unaendelea duniani. Makadirio hayo ni asilimia 0.2 zaidi ya makadirio yaliyotolewa mwezi Juni mwaka jana.
Benki hiyo imesema mwaka huu utakuwa ni mwaka wa kwanza tangu
utokee msukosuko wa kifedha duniani, kwa uchumi wa dunia kuendelea
katika uwezo kamili. Mwaka jana ongezeko la uchumi wa dunia lilifikia
asilimia 3, na kuwa la juu zaidi tangu mwaka 2011, na ongezeko kubwa
kuliko la asilimia 2.4 la mwaka 2016, ambalo lilikuwa kubwa zaidi tangu
kutokea kwa msukosuko wa kiuchumi.
Kutokana na uwekezaji mkubwa binafsi nchini Marekani, uchumi wa nchi hiyo kwa mwaka jana ulitarajiwa kukua kwa asilimia 2.3. Benki ya dunia pia imepandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 6.4, likiwa ni asilimia 0.3 zaidi ya makadirio ya mwezi juni mwaka jana.

0 comments:
Post a Comment