Mkufunzi wa
Borussia Dortmund Peter Stoger anasema kuwa hakuna ombi la kumsajili
Pierre-Emerick Aubameyang lililowasilishwa na Arsenal.
Mshambuliaji
huyo wa Gabon ambaye ananyatiwa na the Gunners, hakusafiri na wachezaji
wenzake kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Hertha berlin ambayo ilikamilika
1-1."hakuna mazungumzo yoyote katika meza kuhusu uhamisho wa Aubameyang ,yanayoendelea ni uvumi. alisema Stoger.
"Tunapanga na Pierre-Emerick Aubameyang na kuna vile atakavyorudi katia kikosi cha kwanza cha timu ."
Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutanoi wa timu.

0 comments:
Post a Comment