Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhe. Doto Mashaka Biteko
kuwa Naibu Waziri wa Madini, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu,
Januari 8, 2018, asubuhi.
Baada ya kuapishwa, Mhe. Dotto Biteko amesema;
“Kwanza namshukuru Mungu kwa siku ya leo na namshukuru kwa kuweza
kutokea haya yote. Nakushukuru wewe Mheshimiwa rais kwa kuweza kuniteua,
sina la kukupa ila kutenda kazi kwa bidii. Mhe. Rais nina bahati kubwa
sana na hata wewe umelishuhudia kwenye mikutano mingi sana, umenipa sifa
kubwa kwa kuhudumu chini ya mwanamke ambaye ni mchapa kazi sana. Niko
tayari kufanya kazi kwa bidii na namuomba Mungu usije jutia uamuzi
wako,” alisema Biteko.
Naye Mhe. Spika Ndugai alipota fursa ya kuzungumza akasema;
“Sisi Bunge tumekuwa tukishauri kwa muda sana kwa serikali kuwa wizara
ya nishati na madini imekuwa wizara kubwa na nzito sana na nashukuru
umeifanyia kazi kwa kuweka wizara mbili za madini na nishati.
Tunakushukuru sana mheshimiwa Rais. Mhe. Dotto ni mchapakazi na ana
utumishi uliotukuka,” alisema Ndugai.
0 comments:
Post a Comment