Waziri wa maswala
ya angani nchini Ghana Cecelia Dapaah ameionya kampuni ya ndege ya
British Airways kwamba huenda ikakabiliwa na vikwazo kufuatia ripoti ya
kunguni katika baadhi ya ndege zake zinazoingia nchini humo.
Gazeti
la Uingereza wiki hii liliripoti kwamba ndege moja ya kampuni hiyo
iliokuwa ikielekea mjini Accra ilizuiwa katika uwanja wa Heathrow kwa
saa kadhaa baada ya wadudu hao kuonekana wakitambaa katika viti vyake.British Airways ambayo ina ukiritimba wa ndege kati ya Uingereza na Ghana imetoa taarifa ikisema kuwa kisa kama hicho sio cha kawaida ma kundi la wataalam limechukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo.
Gazeti la The Sun lilichapisha habari kuwa wahudumu wa ndani ya ndege hiyo walipigwa na butwaa walipowaona kunguni wengi tu ndani ya ndege na kulazimu kuahirishwa kwa safari yao.
0 comments:
Post a Comment