Wednesday 31 January 2018

IOM yaomba msaada dola za kimarekani milioni 103.7 kwa ajili ya Sudan Kusini


Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM limetoa wito wa kutolewa msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 103.7 kwa mwaka huu ili kutoa msaada wa kuokoa maisha, kuunga mkono matibabu na uhamiaji wa watu wanaoathiriwa na migogoro nchini Sudan Kusini. 

IOM inasema mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan Kusini bado ni makubwa, na hali inaendelea kuzorota licha ya juhudi za hivi karibuni za kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya miaka minne nchini humo.

IOM imesema fedha hizo zitatumika kwa watu zaidi milioni 1 waliopoteza makazi, jamii zilizowapokea, na jamii za wakimbizi wenye nia ya kurudi nchini Sudan Kusini.

0 comments:

Post a Comment