Wednesday 31 January 2018

Swansea yaishushia kipigo Arsenal



Katika matokeo ya soka nchini uingereza, klabu ya Swansea City imeendelea kufufua matumaini ya kusalia ligi kuu baada ya ushindi wa jana dhidi ya Arsenal wa magoli matatu kwa moja ulioifanya timu hiyo sasa ipande hadi nafasi ya 16 kwa kufikisha pointi 23 katika 25 ilizocheza msimu huu na wakiwa wamefungwa mechi moja tu kati ya nane tangu wamwajiri kocha mpya Carlos Carvalhal.
Magoli ya Swansea katika mechi hiyo yalifungwa na Clucas, mawili na Jordan Ayew aliyefunga moja, huku goli la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Nacho Monreal.
Katika mechi zingine zilizopigwa jana Westham walitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Crystal Palace na Liverpool ikishinda ugenini kwa magoli 3-0 dhidi ya Huddersfield.
Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi saba, ambapo miongoni mwa mechi hizo, Manchester United wanacheza Ugenini dhidi ya Tottenham na vinara wa ligi hiyo Manchester City watacheza nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion

0 comments:

Post a Comment