Wednesday 17 January 2018

Jose Mourinho kusaini mkataba mpya kuifundisha Manchester United


 Wakala wa Kocha Jose Mourinho, Jorge Mendez ameanza mazungumzo na Manchester United, na huenda mteja wake akaongeza muda katika mkataba wake wa kuifundisha klabu hiyo hadi kufikia mwaka 2021.
Mkataba wa meneja huyo raia wa Ureno unafikia tamati mwezi juni mwaka 2019, lakini kutokana na mipango yake aliyoorodhesha katika nyaraka zake inaonyesha kuwa hana mpango wa kuachana na United katika miaka ya Hivi Karibuni.
Tangu ajiunge na Man United, Mourinho anajivunia mafanikio aliyopata, ikiwemo kombe la Yuropa, Ngao ya Hisani na kombe la ligi, na akiwa na mwenendo mzuri kwenye ligi mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment