Wednesday 17 January 2018

Jeshi la Uganda laapa kutokata tamaa operesheni DRC


Jeshi la Uganda limelaani shambulizi lililofanywa na waasi wa kundi la ADF dhidi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), na kusababisha vifo vya askari watatu na wengine watano kujeruhiwa.
Msemaji wa jeshi la Uganda Bw. Richard Karemire amesema, kitendo hicho cha ADF hakitazuia jitihada za kikanda za kuliondoa kundi hilo. Jeshi la Uganda UPDF litaendelea kushirikiana na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwafukuza wale wanaovuruga amani ya ya kikanda.
Habari zinasema, waasi wa ADF walishambulia kambi ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya Muzambay katika jimbo la Kivu Kaskazini baada kufukuzwa na jeshi la Uganda.

0 comments:

Post a Comment