Kanisa Katoliki nchini DRC limelaani vikali utumiaji
nguvu katika kuzuwia mandamano ya waumini wa kikatoliki ya kumpinga rais
Joseph Kabila.
Kadinali wa Kinshasa Laurent Monsengwo amevitaja vitendo hivyo vya
jeshi na polisi kuwa vya ukatili. Monsengwo ameukosowa pia utawala wa
rais Joseph Kabila ambao ameuelezea kuwa usiojali raia wake na
unaojirundikia mali za umma.Polisi kwa upande wake wamekanusha taarifa
ya utumiaji nguvu uliozidi kiasi na kukanusha idadi ya vifo iliotolewa
na wandalizi wa mandamano hayo.Kiongozi wa kanisa Katoliki mjini Kinshasa, kadinali Laurent Monsengwo alikuwa na matamshi mazito katika kulaani kile alichoelezea kuwa ni ukatili wa maafisa wa jeshi na polisi dhidi ya wandamanaji wa kanisa katoliki.
"Kuwazuwiya waumini kutoingilia kanisani kwa ibada, wizi wa pesa na simu za waumini hao,msako waliofanyiwa na polisi na jeshi.Kuingia kwa wanajeshi hao hadi makanisani ilikuwasaka wale wanaoelezea kuwa ni waletafujo,kuwapiga risasi watu ambao hawakuwa na silaha ni vitendo vya ukatili ambavyo vinatakiwa kusitishwa haraka," kadinali Laurent Monsengwo.
Kadinali Monsengwo amewataka viongozi dhaifu kuondoka ili kuweko na amani na sheria nchini Kongo. Kwenye ujumbe wake huo aliousoma mbele ya waandishi habari, Monsengwo amehoji juu ya dhamana ya viongozi wa taifa.
"Vipi kuwapa imani viongozi wanaokeuka haki za imani ya wananchi wao ? haki hizo ambazo ni msingi wa uhuru wa na haki za binadamu kama alivyoandika baba mtakatifu Benedict wa 16," ameongeza kadinali Laurent Monsengwo.
Kadinali wa Kinshasa ameomba kuweko na uchunguzi wa kina wa machafuko hayo na wahusika kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo kanisa Katoliki halikutaja idadi ya watu waliouliwa au uharibifu uliofanywa kwenye makanisa yake. Waandalizi wa mandamano hayo ya kumpinga rais Joseph Kabila walielezea kwamba ni watu 12 waliouwawa na wengine 140 kushikiliwa na polisi.
0 comments:
Post a Comment