Thursday 4 January 2018

Rais Trump atishia kusitisha msaada Palestina

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha msaada wa thamani ya  dola milioni 300 kwa mwaka kwa Palestina, hatua ambayo imeshutumiwa vikali na viongozi wa Palestina wakisema hawatatetereshwa na vitisho. 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Trump, amesena wanawalipa Wapalestina mamilioni ya dola kwa mwaka na hawapati shukran wala heshima kutoka kwao akiongeza kuwa kutokana na kuwa Wapalestina hawana nia tena ya kufanya mazungumzo kuhusu amani basi hakuna haja kuendelea kuwapa misaada katika siku za usoni.
Haijabainika wazi iwapo Trump anatishia kusitisha bajeti nzima kwa ajili ya Palestina ya kima cha dola milioni 319 au la. Afisa mwandamizi wa Palestina Hanan Ashrawi amesema hawatatishwa na Marekani na kumshutumu Rais Trump kwa kuhujumu azma ya Palstina kutafuta amani, uhuru na haki.
Nabil Abu Rdainah, msemaji wa Rais Abbas amesema Jerusalem haiuzwi, si kwa dhahabu wala fedha akiongeza kusema kuwa Wapalestina hawapingi kurejea katika meza ya mazungumzo ya kutafuta amani yaliyokwama mwaka 2014, lakini kwa misingi ya kuundwa taifa la Palestina kuambatana na misingi iliyokuwepo kabla ya Israel kuuchukua kwa nguvu ukingo wa magharibi, Jerusalem Mashariki na ukanda wa Gaza wakati wa vita vya mwaka 1967.
Marekani imekuwa ikiipa mamlaka ya ndani ya Palestina msaada wa kupiga jeki bajetii yake na w kiusalama pamoja na dola nyingine milionii 304 kwa ajili ya miradi ya Umoja wa Mataifa katika ukingo wa magharibi na Gaza.

0 comments:

Post a Comment