Tuesday 23 January 2018

Liverpool yaanza wiki vibaya,yafungwa kwa mara ya kwanza


Rekodi ya kutofungwa katika mechi nyingi iliyokuwa imeanza kuandikwa na klabu ya Liverpool imefutwa jana ilipofungwa goli 1-0 na Swansea City. Goli la Swansea lilifungwa na Alfie Mawson katika dakika ya 40 ya mchezo huo, na Liverpool ilikuwa haijafungwa katika mechi 18 tangu mara ya mwisho mwezi Oktoba mwaka jana ilipokubali kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa Tottenham.
Katika mechi sita ilizocheza tangu imwajiri kocha mpya Carlos, huu ni ushindi wa kwanza, imepoteza mara moja na imetoa sare mara nne, hivyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika safari yake ya kujinusuru kushuka daraja.

0 comments:

Post a Comment