Tuesday 23 January 2018

Ziara ya Kombe la Dunia Afrika Mashariki, Nairobi ni Februari 25, Kampala Machi 5, na Beijing ni April 25


Ziara ya kutembeza tuzo halisi ya ubingwa wa kombe la dunia kwenye mchezo wa soka imeanza rasmi jana mjini London nchini Uingereza na tuzo hiyo ikitarajiwa kupitishwa katika miji 91 ya mataifa 51 katika mara yote Duniani. Hapa Beijing kombe hilo litapita Aprili 25 kabla ya kwenda Shanghai Aprili 26, kwa nchi za Afrika Mashariki kombe hilo litatua Nairobi nchini Kenya Februari 26, na Kampala Uganda mwezi Machi 5.
Lengo la ziara ya kombe hilo, kwa mujibu wa waratibu ni kuwapelekea kwa ukaribu zaidi wapenzi na mashabiki wa soka kombe halisi, lakini pia ikiwa ni kuitangaza michuano ya kombe la dunia ijayo itakayofanyika nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment