Tuesday 9 January 2018

Oprah Winfrey kuwania Urais

Wakati wa ufunguzi wa tamasha la tuzo za Golden Globe 2018, mwandalizi Seth Meyers alifanya utani wa wazo la uwezekano wa Oprah Winfrey kuanzisha kampeni ya kuwania urais.

Wakati Winfrey aliposimama mbele ya umati wa watu na kutoa hotuba yake haikuwa ya mchezo.
Kuna habari nchini Marekani kwamba ni kweli kwamba anataka kuwania urais.
Kwa miaka kadhaa sasa malkia huyo wa kipindi cha mazungumzo nchini Marekani , amekuwa muigizaji wa filamu na mzalishaji wa vipindi na sasa anamiliki vituo kadhaa vya runinga.
Hotuba yake katika tuzo za Globes ilionekana kuwa ya mgombea wa urais ambaye ameanza kampeni .
Hizi hapa sababu zake.

Alizungumza kuhusu yeye binafsi.

''Mwaka 1964 , nilikuwa msichana mdogo katika sakafu ya nyumba ya mamangu mjini Milwaukee, nikimtazama Anne Bancroft akitoa tuzo ya muigizaji bora katika tuzo za 36 za Academy .Alifungua barua na kusema maneeo matano: Mshindi ni Sidney Poitier''.
Mizizi ya mtu anakotoka , ni swala kubwa katika siasa za Marekani siku hizi , tangu Donald Trump alipowashinda wanasiasa waliojikita katika uchaguzi wa urais uliopita 2016.
Winfrey alianza hotuba yake siku ya Jumapili usiku akikumbuka alivyokuwa msichana mdogo akimtazama mtu mweusi wa kwanza kushinda tuzo ya Academy.
Swala la wanasiasa kuzungumzia kuhusu walikotoka limekuwa likitumiwa na kila mwanasiasa kama njia mojawapo ya kuwaonyesha raia kwamba wao ni Wamarekani waliotoka katika matabaka ya chini licha ya kuwa watu maarufu.
Kwa kuwakumbusha watazamaji alivyoishi akiwa mdogo katika jimbo la Wisconsin, Winfrey aligonga ndipo.
Taarifa iliokuwa na malengo
"Kile ninachojua ni kwamba ukweli ni silaha kubwa tulionayo.."
Ukweli dhidi ya walio mamlakani ni swala jipya katika siasa za Marekani , lakini ni swala lenye athari kubwa..
Bwana Trump alifanya kampeni ya aina yake. Alikuwa mgeni ambaye alikuwa anakabiliana na wanasiasa waliojikita aliodai katika hotuba yake kwamba wamevuna matunda ya serikali huku raia wakigharamika.
Baada ya kuzungumzia kuhusu uhuru wa wanahabari , Winfrey baadaye alizungumza kuhusu wanawake kutoka matabaka tofauti, ikiwemo wafanyikazi wa nyumbani, wale wa shambani , wafanyikazi wa viwandani, madaktari na wanajeshi ambao wamevumilia unyanyasaji.
Iwapo Winfrey atagombea, wapinzani wake watamuona kuwa muigizaji ambaye hajui kinachoendelea katika duniani ya kawaida.
Ni mambo kama hayo ambayo yanaweza kumfanya aonekane kama sauti yenye suluhu.

Historia

"Recy Taylor alifariki siku kumi zilizopita kabla ya kaudhimisha siku yake ya kuzaliwa. Aliishi kama vile tunavyoishi , miaka mingi katika utamaduni uliojaa unyanyasaji chini ya uongozi wa wanaume. Na kwa muda mrefu wanawake hawajasikika ama hata kuaminika iwapo wangejaribu kuzungumza ukweli mbele ya wanaume wenye uwezo mkubwa. Lakini sasa wakati wao umepitwa na wakati.
Katikati ya hotuba yake, Winfrey alisisitiza habari ya Recy Taylor katika hotuba yake ambaye alitekwa nyara na kubakwa na wanaume sita weupe 1994.
Kesi ya Taylor ilichukuliwa na NAACP and Rosa Parks miaka 11 kabla ya kupata umaarufu wa maandamano ya Montegomery dhidi ya mabasi.
Ronald Reagan, wakati wa hotuba yake ya taifa 1980s, alitumia mashujaa wa kibinafsi ili kuelezea maswala yake , mtinndo wa kuzungumza ambao sasa unatumika sana na wanasiasa katika hotuba zao.
Awataka raia kuchukua hatua
"Ninataka wasichana wote wanaotazama hapa sasa kujua kwamba siku mpya iko mbele yenu. Na iwapo siku hiyo mpya itaanza kuangaza itakuwa kwa sababu ya wanawake wengi , ambao wako katika chumba hiki pamoja na wanaume muhimu wanaopigana kuwa viongozi watakaotupepeleka katika wakati ambao hakuna mtu anayeweza kusema Mimi tena.

Eti..Eti..
Wagombea wa urais huja na kuondoka na mwaka wa 2020 uko mbali kisiasa. Iwapo Winfrey anataka kuingia katika siasa, milango ipo wazi.
Hotuba yake sio ajali. Ni njia ya kujijenga kitaifa kutoka kwa mwanamke maarufu ambaye yeye na kikosi chake wana ufahamu kuhusu hasira za raia wa Marekani.
Winfrey anatambulika, ana fedha na iwapo hotuba yake ya jumapili ni ishara , ni ujumbe wa mgombeaji.
Alex Burns wa gazeti la New York Times anauliza ni nani miongoini mwa Democrats anayeweza kumpatia ushindani mkali kwa uteuzi wa chama hicho? Orodha yake hatahivyo ni fupi. Bernie Sanders? Joe Biden? pengine Seneta Elizabeth Warren?
Kweli, Winfrey ni mwanasiasa mpya na wanachama wa Democrats wanaweza kuamua kwamba baada ya miaka minne ya Trump, raia wa Marekani wangependa kumchagua mgombea mwenye mazoea ya uongozi.
Ijapokuwa rais Trump alikuwa amejihami katika kipindi chake chote cha kampeni ,haijulikani ni vipi Winfrey ataweza kujimudu katika nyanja za kisiasa.
Na huku akiwa sauti ya Wamarekani wa daraja la katikati wakati wa kipindi chake cha mazungumzo , uhusiano wake na waigizaji maarufu wa Hollywood huenda ukamtia mashakani kisiasa.
Iwapo siku yake mpya itaangaza huenda watu maarufu na wanasiasa wakawa na uhusiano mkubwa.
Iwapo rais Trump amebadilisha mtindo wa rais mpya wa Marekani na mkakati wa kuelekea Ikulu ya Whitehouse , basi usiku wa Jumapili iliopita huenda ndio mwanzo wa kampeni isio ya kawaida 2020.

0 comments:

Post a Comment