Thursday 18 January 2018

Rafael Nadal azidi kung'ara mashindano Australia

 
Mchezaji nyota wa Tennis Rafael Nadal wa Hispania amefanikiwa kufuzu raundi ya tatu katika michuano ya Australia baada ya kumfunga Leonardo Mayer wa Marekani kwa seti ya 3-0 yenye alama 6-3 6-1 na 7-6 mjini Melbourne. Kutokana na umahiri wa Mayer, imemchukua saa 2 na dakika 38, Rafael Nadal kushinda mechi hiyo ambayo licha ya matokeo kumbeba Nadal, Mayer ndiye aliyeongoza kwa takwimu za awali.
Kwa ushindi huo, Rafael Nadal ambaye ni bingwa mara 17 wa michuano mikubwa ya tennis, anatarajiwa kukutana na Damir Dzumhur wa Bosnia siku ya ijumaa

0 comments:

Post a Comment