Friday, 5 January 2018

Mohamed Salah wa Misri anyakua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017



Kama ambavyo wengi walitabiri kutokana na mafanikio aliyopata akiwa na timu yake ya taifa pamoja na klabu, Mohamed Salah wa Misri ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017 akiwashinda wenzake Sadio Mane aliyeibuka mshindi wa pili na Pierre Emerick Aubameyang aliyeshinda nafasi ya tatu. Mwaka 2017, Salah amejipambanua baada ya kuisaidia Liverpool aliyojiunga nayo akitokea AS Roma ya Italia, kwa kuifungia magoli 23 katika mechi 29 alizocheza, lakini zaidi akiisaidia timu yake ya taifa ya Misri kuweka historia iliyofutika miaka 25 iliyopita ya kufuzu kombe la dunia.
Hii ni kubwa ya tatu ya kimataifa ya nyota huyo katika baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora kutoka mataifa ya kiarabu, mchezaji bora wa Afrika wa Tuzo za BBC.
Katika tuzo za jana zilizofanyika mjini Accra nchini Ghana, Mwanadada Asisat Oshola alishinda tu Soka, Uingereza:zo ya mchezaji bora kwa wanawake na mchezaji bora chipukizi akiibuka Patson Daka kutoka Zambia.
Timu ya taifa ya Misri ilitangazwa kuwa timu bora ya mwaka kwa wanaume na timu ya wanawake ya Afrika Kusini ikitangazwa timu bora ya mwaka 2017.
Wydad Casablanca ya Morocco ndiyo klabu bora ya soka ya mwaka na kocha Hector Cuper wa timu ya taifa ya Misri akitangazwa kocha bora wa mwaka 2017.
Lakini tuzo za heshima kwa viongozi na watu mashuhuri, Mzee Ibrahim Sunday ambaye alikuwa mchezaji maarufu kutoka Ghana katika miaka ya 66, Nyingine ilikwenda kwa Ahmed Yahya wa Mauritania aliyetangazwa kiongozi bora wa soka.
Wengine waliopewa tuzo ya heshima ya juu ni Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ambaye alihudhuria hafla hiyo ya utoaji tuzo, pamoja na George Weah ambaye ni mwanasoka wa zamani na Rais Mpya wa Liberia.

0 comments:

Post a Comment