Mechi hiyo inafanyika katika uwanja wa Olimpiki el Menzah mjini Tunis, na itatoa tathmini halisi ya maandalizi ya kikosi cha kocha Antoine Hey kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano.
Rwanda tayari wamecheza mechi mbili za maandalizi, moja ikiwa ni dhidi ya Sudan ambayo ilidumu kwa dakika arobaini tu jumamosi iliyopita baada ya wachezaji kuzozana na nyingine iliyoisha kwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Namibia siku ya jumapili.
Timu hiyo inatarajiwa kuelekea Morocco kesho kwa ajili ya mashindano ambako iko kundi C paomja na timu za Libya, Nigeria na Equatorial Guinea.
0 comments:
Post a Comment