Kampuni ya bima ya afya nchini ya AAR kwa kushirikiana na Jema Foundation inayojikita katika kutoa elimu kwa umma kuhusu ugonjwa wa saratani ya Mitoke ijulikanayo kama (Hodgkin’s Lymphomo), wametoa msaada kwa watoto wanaopata matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kupitia kwa shirika lisilo la kiserikali la Tumaini La Maisha Tanzania, ambalo limejikita katika kusaidia matibabu ya watoto wenye saratani nchini kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili chini ya Wizara ya Afya.
Wafanyakazi
wa Bima ya Afya ya AAR na timu nzima ya Jema foundation wakiiwa na
watoto walioathirika na Saratani,walipoenda watemebelea na kutoa msaada
wao,hospitalini Muhimbili
Afisa
Mahusiano wa AAR Bi Hamida Rashid kushoto kwake ni Meneja Mauzo wa AAR
Bi Tabia Massudi na Bi Jema wakikabithi msaada kwa Mzazi,Mama Evans, na
Bi Lilian na Bwana Alex wawakilishi wa Tumaini La Maisha
“Kama bima ya afya inayoongoza na kutoa huduma bora, lengo la AAR ni kuhakikisha jamii inayotuzunguka inakuwa na afya bora. Tunatambua juhudi kubwa inayofanywa na Serikali,Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na shirika la Tumaini La Maisha Tanzania katika kusaidia kupambana na saratani kwa watoto. Hivyo, tumeamua kuunga mkono juhudi hizi kwa vitendo kwa kusaidia sehemu ya mahitaji kwa watoto hawa. Kwetu sisi watoto ni sehemu muhimu ya moyo wa Taifa,” amesema Bi. Rashid.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jema Foundation,Bi Jema Baruhani akikabidhi zawadi
walizowaandalia watoto,walipoenda kuwatembelea Hospitalini Muhimbili
katika jengo la Ujasiri
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha Tanzania, Dkt. Patricia Scanlan amewashukuru AAR na Jema Foundation kwa msaada huo na kutoa wito kwa mashirika na watu binafsi kuiga mfano huo.
“Ninawashukuru sana AAR na Jema Foundation, ni hatua nzuri walioichukua. Saratani kwa watoto inamgusa kila mmoja kwenye jamii yetu. Tunapo wasaidia watoto hawa tunalisaidia Taifa zima” Amesema Dkt Scanlan
“Tunahudumia watoto zaidi ya 600 kwa mwaka wenye saratani hapa Muhimbili, wana mahitaji mengi. Jamii inapotuunga mkono kama hivi ni ishara ya ushindi katika kuokoa maisha ya watoto hawa,” aliongeza .
Dkt. Scanlan ametoa wito kwa jamii kuhakikisha inatoa kipaumbele kwa afya ya watoto kwa kuwapima saratani kwani wengi upoteza maisha kwa kuchelewa kupata matibabu husika kutokana na kutojua hali zao mapema.
0 comments:
Post a Comment