Golikipa
Eric ndayishimiye wa Rwanda jana amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kupambana na hatari zilizokuwa zikiletwa langoni kwake na washambuliaji
machachari wa timu ya Taifa ya Nigeria na kuupeleka mchezo wao wa kwanza
wa kundi C la mashindano ya kombe la mataifa ya Africa kwa wachezaji wa
ligi za ndani kuisha kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.
Licha ya umahiri wa Nigeria wa kumiliki mechi hiyo, vijana wa Amavubi
wakiongozwa na Djihad Bizimana (aliyetangazwa mchezaji bora wa mechi)
walimudu kuwianisha umiliki wa mpira kati ya pambe mbili hizo.
Baada ya kuanza vizuri mechi hiyo, Rwanda sasa ili waweze
kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele watalazimika kupata matokeo
mazuri katika mechi ijayo watakapocheza na Equatorial Guinea siku ya
alhamisi mjini Tangier.
Katika mechi nyingine ya kundi C iliyopigwa jana Libya walishinda kwa magoli 2-0 dhidi Equatorial Guinea.
Na michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili za kundi D
zitakazopigwa mjini Agadir, ambako Angola watacheza na Burkina Faso,
huku Cameroun dhidi ya Congo-Brazzaville.
0 comments:
Post a Comment