Monday 15 January 2018

Ryan Giggs kuchukua nafasi ya Chris Coleman timu ya taifa Wales

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa wa Wales Ryan Giggs anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales kwa mkataba wa miaka minne.

Chama cha soka cha nchini Wales (FAW) kiliwafanyia usaili Craig Bellamy, Osian Roberts, Mark Bowen na Ryan Giggs ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Chris Coleman aliyekwenda kuifundisha klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.
Kati ya majina yote hayo, Giggs ameonekana kuwa anafaa kwa nafasi hiyo, hivyo FAW itamtangaza leo katika mkutano na waandishi wa habari.

0 comments:

Post a Comment