Monday 15 January 2018

Jeshi la Sudani limejipanga kukabiliana na tishio la usalama

 

Sudan imesema jeshi lake liko tayari kukabiliana na tishio lolote la usalama linaloweza kutokea kwenye eneo la mpaka wa mashariki mwa nchi hiyo.

Akikutana na mwenzake wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu, waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amesema, wamegundua kuwa kuna nchi inajaribu kuwadhuru, na jeshi la Sudan limepanga upya vikosi vyake ili kukabiliana na kitendo chochote kitakachoharibu usalama wa Sudan.
Kwa upande wake Bw. Gebeyehu amesema, Ethiopia inapenda kukuza uhusiano wa pande mbili kati yake na Sudan, na kuendelea kusaidia kuhimiza amani katika kanda hiyo.

0 comments:

Post a Comment