Thursday 25 January 2018

TFF yamtangaza mwamuzi wa mechi ya Azam na Yanga


Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ,limetegua kitendawili kuwa mwamuzi gani atachezesha mechi baina ya miamba ya soka ya nchini humo Azam fc na Yanga itakayopigwa jumamosi ijayo mjini Dar es Salaam. Mwamuzi wa kati atakuwa Isreal Nkongo, atakayesaidiwa washika vibendera Josephat Bulali na Soud Lila, mwamuzi wa akiba atakuwa Elly Sasii na Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.
Yanga inazidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya vinara, Simba SC wenye pointi 32.

0 comments:

Post a Comment