Timu
ya taifa ya Uganda ishuka uwanjani leo kucheza na Namibia katika mechi
yake ya pili ya hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Uganda ambayo iko kundi B, leo itahitaji ushindi itakapocheza dhidi
ya Namibia ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali,
kwa kuwa tayari ilikwisha poteza kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Zambia.
Mechi nyingine ya Kundi B, itazikutanisha Ivory Coast na Zambia,
lakini katika kipekee kutoka kundi A la mashindano hayo, Morocco na
Sudan zimefuzu hatua ya robo fainali baada ya ushindi zilioupata katika
mechi za pili za hatua ya makundi.
Morocco ilishinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Guinea ya Conakry, Sudan ikishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Mauritania
0 comments:
Post a Comment