Wagombea
27 wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika
uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo
mawili ya ubunge na kata nne.
Katika
uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, mgombea udiwani kupitita CCM
katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani
Dodoma, amepita bila kupingwa.
Mbali
na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za
Tanzania Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku
ya Jumatano ya tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa
kushiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.
Akizungumzi
uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa
baada ya mgombea wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.
Amesema
katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa
jimbo hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza
kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya (SAU) na Mwajuma Milambo
kutoka UMD.
Mkunga
amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya
(Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.
Wengine
ni Salim Mwalimu (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa
(NRA), George Christian (CCK), Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na
Ashiri Kiwendu wa AFP
Kuhusu
uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro,
Mkunga amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel
(CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis
Christopher MosiwaCHADEMA.
Katika
kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha
wagombea ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM,
na CHADEMA.
Amevikumbusha
vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha
kampeni kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na
kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Februari
mwaka 2018.
Na Hussein Makame-NEC
0 comments:
Post a Comment