Wednesday 31 January 2018

Umoja wa Mataifa waipongeza Ethiopia kwa kulinda amani


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Bw Jean Pierre Lacroix ameipongeza Ethiopia kwa juhudi zake kwenye kazi za kulinda amani duniani.
Bw. Lacroix amesema hayo alipozungumza na waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw Workneh Gebeyehu mjini Addis Ababa.
Bw Lacroix amesema walinzi wa amani wa Ethiopia wamepata mafanikio walipofanya kazi katika Tume ya Umoja wa Mataifa huko Abyei UNISFA, ambao wameaminiwa na pande zote za vita. Pia ametoa wito kwa serikali ya Ethiopia itoe mchango zaidi kwenye vikosi vya kulinda amani.
Bw. Gebeyehu amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mfumo wa usalama na amani nchini Somalia na Sudan Kusini.

0 comments:

Post a Comment