Wednesday 31 January 2018

Usain Bolt aikacha riadha,ajiunga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini


Mwanariadha maarufu zaidi duniani, raia wa Jamaica Usain Bolt, jana amejiunga rasmi na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mazoezi katika uwanja wao wa mazoezi wa Chloorkop jana jumatatu.
Mabingwa hao wa soka Afrika wa mwaka 2016 walitangaza kuwasili kwa Bolt kupitia Twitter na kupakia video ya Mjamaica huyo akifanya mazoezi na wachezaji.
Bolt amealikwa kufanya mazoezi wiki moja na klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwezi Machi na anapanga kukubali mwaliko huo.
Bolt alistaafu riadha Agosti mwaka jana baada ya mashindano ya ubingwa wa dunia jijini London mara nyingi amekuwa akionyesha nia ya kujiunga na kandanda.

0 comments:

Post a Comment