Mwanamume mmoja
ametoroka nchini Burundi baada ya kuwapa adhabu ya kikatili watoto wake
wawili ambao inadaiwa aliwapata wakiiba mahindi kwenye shamba lake.
Mwanaume huyo aliwazika ardhini wanawe wawili hadi sehemu ya vifua kabla ya kuwachapa viboko. Walibahatika kuokolewa na mpita njia ambaye alikuwa jirani yao .
Taarifa zinasema watoto hao wenye umri kati ya miaka 8 na 10 walikamatwa wakiwa wanaiba katika shamba la mahindi.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa hawajui ni nini kingetokea kwa watoto hao kama jirani yao asingepita.
Mwanaume huyo kisha alitoroka na watoto hao wakaokolewa.
Polisi wanasema bado wanamsaka mwanaume huyo kwa ajili ya kumfikisha mbele ya sheria.
Si mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kikatili dhidi ya watoto kufanyika nchini Burundi.
Watoto wawili walikatwa mikono yao ya kushoto katika jimbo la kati la Gitega mwezi Novemba mwaka jana baada ya kupatikana wakiiba mahindi.

0 comments:
Post a Comment