Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe jana
Januari 20, 2018 amemtembelea na kumjulia hali msanii wa filamu Wastara
nyumbani kwake Tabata Sanene, Dar es Salaam.
Wastara
kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu na yupo
kwenye maandalizi ya safari kwenda India kwa matibabu zaidi.
Waziri
Mwakyembe akiambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Katibu
Mtendaji wa BASATA alimtakia kheri Wastara na kumkabidhi mchango wa Shs.
1,000,000/= (milioni moja).
Aidha,
Mwakyembe aliwasihi wasanii na Watanzania kwa ujumla kumchangia Wastara
kwa hali na mali ili aweze kupata fedha za kumwezesha kwenda India kwa
matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment