WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto
akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed
Kidiwa
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa
vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya
zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo
inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi
daraja la kwanza msimu ujao.
Makabidhiano
hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati
wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya
ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo
kuweza kufikia malengo yao.
Aliyasema
hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa
iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African
Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo
inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu
ujao inarudi Ligi kuu.
“Niseme
tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano
ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union
lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la
kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema
Akizungumza
baada ya kupokea vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu ya African
Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada
huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na
changamoto hiyo kwisha.
Alisema
msaada uliotolewa na Waziri utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia
malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio
ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.
“Mh
Waziri tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana
na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na
hatimaye ligi kuu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
0 comments:
Post a Comment