Thursday, 22 February 2018

Ahukumiwa miaka 93 jela kwa kughushi nyaraka



Mahakama imemhukumu kwenda jela jumla ya miaka 93(Miaka mitatu kwa kila kosa) aliyekuwa mfanyakazi wa CRDB, Telesphory Gura baada ya kumkuta na hatia ya makosa 31 ambapo 29 yanahusu kughushi nyaraka na mawili ya wizi wa milioni 29.8

Aidha, Mahakama imemtia hatiani kwa kosa la kutakatisha Sh. milioni 29.8 na kumuadhibu kulipa faini ya Sh. milioni 100, ambapo asipolipa atakwenda jela miaka mitano
Baada ya hukumu, Telesphory Gura alidai kuwa amekaa mahabusu kwa miaka mitatu, ana familia ya mke na watoto watatu wote wadogo na wanamtegemea. Pia ana matatizo ya mgongo na shinikizo la damu, hivyo ameomba aangaliwe kwa jicho la huruma!

Hakimu Simba(aliyetoa hukumu) alisema kwamba Mahakama imezingatia maombi ya mshtakiwa
Telesphory Gura anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Agosti 2014 na 2015

0 comments:

Post a Comment