Baada ya kuwepo
kwa sintofahamu ya Cameroon kuwa wenyeji wa fainali za AFCON mwaka
2019 michuano ambayo inayotarajiwa kuanza June saba hadi Julai saba,
kutokana na kutokuwepo kwa kimiundombinu mizuri na maswala ya
uchumi kuweza kuandaa michuano hiyo , CAF ililazimika kufanya
uchunguzi wa maandali zi hayo.
Baada ya CAF kumaliza kufanya
uchunguzi hatimaye wametoa ruhusu kwa Cameroon kuendelea kufanya
maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo baada ya timu ya maafisa wa CAF
kuridhishwa na maandalizi yanayoendelea nchini humo.Juniour Binyam ni mwenyekiti wa kamati ya masuala ya habari wa CAF amethibitisha hilo na kusema kwamba CAF kwa sasa hawana mashaka juu ya maandalizi ya michuano hiyo na wanaona hadi kufika wakati huo Cameroon watakuwa tayari.
0 comments:
Post a Comment