Friday 23 February 2018

HISPANIA-Polisi auwawa akituliza vurugu baada ya mechi



Afisa Polisi mmoja amefariki hapo jana kufuatia vurugu zilizofanywa na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Spartak Moscow dhidi ya wale wa timu ya Athletic Bilbao kabla ya mchezo wa Europa League
Askari huyo alifariki baada ya kufikishwa hospitalini kwaajili ya matibabu kufuatia kupata shinikizo la moyo wakati akijaribu kutuliza vurugu za mashabiki

Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuwasha baruti katika mitaa zilizosababisha baadhi ya mashabiki kufikishwa hospitali
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limesema kuwa limesikitishwa na tukio hilo na linafanya mawasiliano na mamlaka za ndani kupata taarifa zaidi

0 comments:

Post a Comment