Tuesday 27 February 2018

Jaji mkuu Prof Ibrahim azitaka mahakama kutoa nakala za hukumu bure



Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma amewaagiza Mahakimu wote nchini kutoa bure nakala za hukumu kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa haki

Kiongozi huyo mkubwa amewaambia Mahakimu hao kuwa endapo watakutana na kikwazo cha Sheria au Kanuni katika kutekeleza agizo hilo wasisiste kumpelekea mapendezo yao

Alisema ni haki ya kila Mwananchi aliyekuwa na kesi mahakamani kupatiwa nakala ya hukumu yake ndani ya siku 21 tangu kusomwa kwa hukumu hiyo
Nakala ya hukumu imekuwa ikilipiwa kiasi cha shilingi 10,000 kama gharama ya uandaaji wa nakala hiyo
Aidha, Akizungumzia maboresho ya huduma za Mahakama, Prof. Juma alisema Mahakama inao mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea(Mobile Courts) ili kutatua changamoto ya upungufu wa Mahakama kwenye baadhi ya maeneo nchini

0 comments:

Post a Comment