Sunday 11 February 2018

KUTOKA FERNANDO TORRES MPAKA OLIVIER GIRUOD.


Na  Raphael Mwenda.
            Mnamo march 2 mwaka 1969 kampuni ya BAC ambayo ilibadilishwa jina na kuwa BAE System ya nchini marekani ilitengeneza ndege iitwayo CONCORDE iliyokua ikifanya safari zake kutoka uingereza kwenda mataifa mbalimbali inaaminika kuwa Concorde ndio ndege iliyokua kasi zaidi duniani na mpaka leo hii hakuna ndege iliyokua kasi zaidi ya Concorde. Mnamo mwaka 2003 Concorde iliachakufanya kazi baada ya wateja kushuka kiwango kutoka na ajali mbaya iliyotokea mwaka huo na kuua jumla ya watu 113 ikiwamo 109 wote waliokua ndani ya ndege pamoja na wanne waliokua nchi kavu.
           Wakati Concorde ikiacha kufanya kazi mwaka 2003 kule jijini London kuna mrusi mmoja mwenye kiburi majivuno na asitaka utani katika kazi alikua akiinunua klabu ya Chelsea anafahamika kwa majina Roman Arkadyevich Abramovich mfanyabiashara maarufu sana kutoka Russia. Aliichukua Chelsea ikiwa haijawahi kushinda taji la ligi kuu uingereza kwa kipindi kirefu sana aliichukua Chelsea ikiwa inajikongoja kwenda katika ubora. Alihitaji kuifanya Chelsea kuwa timu kubwa kama Manchester United na Real Madrid. Akianza kwa kuwajengea kiwanja kizuri cha mazoezi pale Cobham walipo mpaka leo.
           Katika msimu wake wa kwanza Chelsea ilishika nafasi ya pili kutoka ya nne msimu uliopita na kufika katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa wakitolewa na mabingwa wa kipindi hicho Fc Porto chini ya José Mourinho. Kwa Chelsea yalikua mafanikio makubwa sana lakini kwa Roman Arkadyevich Abramovich yalikua maumivu makubwa sana. Ndio Roman Arkadyevich Abramovich hapendi kufungwa hatamani kuwa msindikizaji wa wengine daima anaamini yeye ni mshindi ama kwa amani fedha hata mtutu wa bunduki.
          Msimu wake wa pili pale Stanford bridge aliamua kumleta José Mourinho akichukua nafasi ya Claudio Ranieri alietimuliwa,Roman Arkadyevich Abramovich akitaka Chelsea iwe timu ya mataji hasa. Katika hili alifanikiwa kwani katika msimu wa 2004-2005 Chelsea ilishinda taji la ligi kuu ya uingereza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 na la kwanza katika historia ya klabu hiyo. Hawakuishia hapo msimu uliofuta pia walichukua ubingwa wa uingereza kwa mara ya pili mfululizo pamoja na kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara kadhaa.
             Lakini pamoja na yote hayo bado Roman Arkadyevich Abramovich hakuridhika alihitaji Chelsea icheze Mpira wa pasi nyingi magoli mengi yaani wapinzani waogope kabisa kukutana na Chelsea. Lakini mbinu za kocha José Mourinho za kulinda sana na kwa njia yoyote ile tupate matokeo hazikumpendeza hivyo alimfutilia mbali na kazi ile kupewa Luis Phillipe Scolari fundi aliempa Ronaldinho Gaucho nafasi ya kuonyesha uwezo kule Japan.
               Roman Arkadyevich Abramovich hakufanya haya kwa maneno bali vitendo zaidi vilihusika alinunua wachezaji wakubwa na kwa bei mbaya ni nani aliemsahau Andriy Shevchenko aliesajiliwa kwa rekodi ya uhamisho pale uingereza akitokea Ac Milan nani kamsahau Didier Drogba kutoka Olympic de Marseille Ricardo Carvalho pia vipi kuhusu usajili wa dunia wa Fernando Torres kutoka Liverpool kwa bei ya kutisha kwa wakati ule paun milioni 50 .
              Concorde ilikua na uwezo wa kutoka pale Heathrow Airport nchini uingereza mpaka kule Canberra Airport nchini Australia kwa muda wa masaa yasiyozidi matano ilikua kasi isiyo ya kawaida ndio maana baada ya ajali ile pale Paris nchini ufaransa iliua abiria na wahudumu wote ndani ya ndege ile. Lakini Concorde haikua kasi kama sekunde za mshale wa maisha uendavyo maisha yapo kasi kuliko kitu chochote kile ulimwenguni baada ya matanuzi na maonyesho ya ubabe pale uingereza hatimae Chelsea ile ile ya     Roman Arkadyevich Abramovich iliyo mnunua Torres kwa rekodi ya ligi iliyomchukua Willian mdomoni kwa Tottenham iliyowanyang'anya Liverpool Salah kutoka Basel iliyomchukua Juan Cuadrado mikononi mwa Manchester United imekwenda kumsajili Olivier Giroud kutoka katika benchi la Arsenal.
                  Antonio Conte kocha pale Chelsea analalama kutopewa kile anachohitaji analia kuwa na kikosi kidogo anadai hana wachezaji stahiki kuchezea chelsea. Yupo sahihi Zappacosta si mchezaji wa kuvaa uzi wa bluu Tiemoue Bakayoko hana thamani ya kakaa katika eneo la mfalme Frank Lampard Ross Barkley ni mzuri lakini si mchezaji sahihi pale Stanford bridge achilia mbali Danny Drinkwater kumbukumbu yangu ndogo inanikumbusha kipindi Ivanovic anatoa jasho José Bosingwa katika ubora wake alikua anakaa benchi Ryan Bertrand aliondoka akikimbia benchi kutokana na nafasi yake kuwa na watu wenye uwezo achilia mbali Kelvin de Bruyne na Mo salah waliokimbia benchi pia kipindi Didier Drogba anacheza paun milioni 50 Torres alikua akikaa benchi.
                  Sijajua tatizo linalofanya leo hii Chelsea iwe na msaada wa (mchezaji wa pili) ambae ameshindwa kuishi katika maisha sahihi kule atokako. Alvaro Morata anasumbuliwa sana na majeraha na hajazoea vizuri mazingira ya uingereza lakini msaada wake kuwa Olivier Giroud kidogo inanipa shaka. Kama tatizo ni     Roman Arkadyevich Abramovich hatoi hela za kutosha au ni Antonio Conte anachagua wachezaji wa aina hii.
                  Mwanamuziki Justine Beiber katika kibao chake cha "Love Yourself" kuna mahala anasema "my mama don't like you and she likes everyone"(mama yangu hakupendi anampenda kila mtu) sidhani kama Antonio Conte ameifanyia makubwa Chelsea kuliko José Mourinho sidhani kama anakitu cha ziada kama mtaliano mwenzie Di Matteo aliewapa Chelsea ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya pale Stanford bridge mashabiki watamshangilia na kumuimba yeyote atakaeletwa kufundisha timu ya haijalishi tatizo ni la Conte ama     Roman Arkadyevich Abramovich hivi ndivyo kasi ya maisha ilivyo wacha siku zisonge.

0 comments:

Post a Comment