Friday 9 February 2018

Makamu wa Rais wa Marekani aweka mgomo kula na dada wa Kim Jong Un


Makamu rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.
Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi.

0 comments:

Post a Comment