Monday 5 February 2018

MAMBO 3 YANAYOJIANDAA KUNYANG'ANYA FURAHA YAKO LEO.


1)Mtema Sumu:Kutoka kusikojulikana kuna watu huwa wanaibuka na kusema maneno ambayo yatakusabisha uvurugike kwenye akili.Mara Nyingi maneno haya huwa yanapelekea kukufanya ujione hauna thamani ama kukuonyesha kuwa hakuna njia ya kufanya kutatua changamoto yako.UWE MAKINI NAO,USIRUHUSU MANENO YAO YAINGIE MOYONI MWAKO.
2)HABARI MBAYA:Kuna wakati habari mbaya zinajiandaa kukufanya wiki nzima isiwe na furaha.Mara nyingi habari hizi zinakuwa ni zile zinazowahusu watu watu wa karibu sana.Zinaweza kuhusiana na ugonjwa,Ajali n.k Fanya maamuzi kuwa hautajikita Katika KULALAMIKA bali kwa habari yoyote MBAYA utajikita kwenye KUITATUA.
3)JIBU LA HAPANA:Inawezekana umekuwa unasubiria jibu kwa jambo Fulani ambalo unalitafuta na umekuwa na matumaini kuwa utalipata.Ghafla bila kutarajia unapata jibu la HAPANA;Usipokuwa mwangalifu Furaha yote itapotea.Kumbuka,HAPANA,haimaanishi wewe sio BORA ama Utapata Kitu Kizuri zaidi.Kila hapana inamaanisha JARIBU TENA na pia KUNA BORA ZAIDI ya hicho ulichoambiwa HAPANA.
Naamini ukikutana na lolote kati ya haya wiki hii hayatakunyan'ganya Furaha yako. (KUJIFUNZA NAMNA YA KUWA NA FURAHA SIKU ZOTE TEMBELEA YOUTUBE CHANNEL YANGU)
See You At The Top
Na  Joel Nanauka
#TIMIZAMALENGOYAKO

0 comments:

Post a Comment