Monday 5 February 2018

Misri na Sudan kufanya mkutano kumaliza mzozo kati ya


Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Ahmed Abu Zeid ametangaza kuwa, Misri na Sudan zitafanya mkutano wa ngazi ya juu Alhamisi wiki hii mjini Cairo, kujadili njia za kuboresha uhusiano kati yao.
Mkutano huo unalenga "kujadili mwelekeo wa uhusiano wa nchi hizo mbili na uratibu kati yao juu ya masuala kadhaa ya kikanda zinayoyafuatilia kwa pamoja".
Amesema mkutano huo utafanyika kwa kufuata maelekezo ya rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na mwenzake Omar al-Bashir wa Sudan baada ya mazungumzo kati yao yaliyofanyika kando ya wakati wa Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofungwa hivi karibuni huko Addis Ababa.

0 comments:

Post a Comment