Monday 5 February 2018

Mkenya avunja rekodi ya Afrika kwenye mbio za mita 800

 


Emmanuel Korir wa Kenya ameweka rekodi mpya ya Afrika ya riadha katika mita 800, alipotumia dakika moja na sekunde 44, nukta 21 na kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka 2014 ya dakika moja na sekunde 44, nukta 52 na mwanariadha Mohamed Aman wa Ethiopia.
Katika hatua nyingine Korir amevunja rekodi ya kitaifa ya Kenya ya kutumia dakika 1 sekunde 44 nukta 71 iliyowekwa na Joseph Mwengi mwaka 2004.
Kori alilitimiza hilo aliposhinda ubingwa wa mbio za kimataifa za Marekani mjini New York.

0 comments:

Post a Comment