Padri Sebastian Yebo adaiwa kutekwa nyara na maafisa
polisi muda mfupi baada ya kumalizika misa aliyokuwa akiiongoza katika
parokia ya mtakatifu Robert mashariki mwa mji wa Kinshasa
Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo polisi inatajwa kumteka nyara
padiri hii leo baada ya misa ya Jumamosi mjini Kinshasa.Hayo yameelezwa
na walioshuhudia wakati nchi hiyo ikiwa katika wasiwasi na mvutano
mkubwa baina ya kanisa na serikali kuhusiana na hatua ya rais Kabila ya
kukataa kuondoka madarakani.Padri Sebastien alichukuliwa mateka na polisi muda mfupi baada ya kumalizika misa mtawa wa kanisa la parokia ya Mtakatifu Robert aliwaeleza waandishi habari wa shirika la AFP katika mji wa Nsele mashariki mwa mji mkuu Kinshasa. Gari ya polisi ilionekana katika maeneo ya kanisa hjilo na maafisa kadhaa kuteremka kwenye gari na kuanza kumpiga padri huyo alisikika akieleza mtawa mwingine ambaye pia alishuhudia tukio hilo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa maafisa hao wa polisi walimsukuma padri huyo na kumuingiza ndari ya gari aina ya Jeep na kuondoka nae huku ikielezwa na watawa hao kwamba alikuweko mtu wasiyemfahamu aliyekuwa akichukua vidio ya padri huyo kupitia simu ya mkononi wakati misa ilipokuwa ikiendelea. Hata hivyo polisi imekataa kutoa maelezo yoyote hadi wakati huu kuhusu kisa hicho baada ya kutafutwa na AFP. Padri Sebastian Yebo amefanya kazi katika parokia ya hiyo tangu mwezi Agosti mwaka 2017.
Rais Kabila mwenye umri wa miaka 46 amekuwa madarakani toka mwaka 2001 chini ya serikali ambayo inakosolewa kwa ufisadi,ukandamizaji na uzembe.Muda wake kwa mujibu wa katiba ulimalizika Desemba mwaka 2016 lakini ameendelea kubakia madarakani hali ambayo inasababisha umwagikaji damu katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo:
0 comments:
Post a Comment