Wednesday 28 February 2018

Roger Federer anyakua tuzo ya mwanamichezo bora duniani kwa mwaka 2017


Mchezaji  na moja wa tennis kutoka Uswisi Roger Federer jana ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika mjini Monaco nchini.
Katika tuzo hiyo Federer aliwashinda Cristiano Ronaldo soka Ureno, Mo Farah riadha Uingereza, Chris Froome mwendesha baiskeli wa Uingereza, Lewis Hamilton wa Formula 1 Uingereza, na Rafael Nadal mcheza tennis wa Hispania.
Pamoja na tuzo hiyo, Federer pia ameshinda tuzo ya mwanamichezo aliyefanikiwa kurejea kwenye ubora wake mwaka 2017 baada ya kupoteza mafanikio kwa muda mrefu kupita, kutokana na kushinda michuano mikubwa ya tennis ya Uingereza na Australia ikiwa ni baada ya miaka saba kupita.
Kwa upande wa wanawake tuzo hiyo ilikwenda kwa mchezaji wa tennis pia Serena Williams.
Timu bora ya michezo-Mercedes ya F1, Timu iliyohusika katika tukio lililovuta hisia-Chapecoense.
Mwanamichezo aliyeshinda tuzo maalum kutokana na mchango wake katika ushiriki wa michezo-Francesco Totti.

0 comments:

Post a Comment