Wednesday 7 February 2018

wanamichezo 32 wa Urusi wakata rufaa kwa katazo la kushiriki mashindano ya Korea


Wanamichezo 32 kutoka Urusi wamekata rufaa baada ya kutoruhusiwa kushiriki mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini.
Miongoni mwao ni wale ambao walifunguliwa na Mahakama ya usuluhishi michezoni CAS kutoka vifungo vya maisha walivyokuwa wafungiwa kutokana na kashfa ya matumizi ya kuongeza nguvu iliyopigwa marufuku michezoni.
Kamati teule ya Olimpiki inakaa leo jumatano kujadili hatma yao ikiwa ni siku mbili tu zimesalia kuanza kwa mashindano hayo mjini PyeongChang.

0 comments:

Post a Comment